Katika Kufikia Mafanikio.
Katika kitabu
cha “The Great Escape”, mwandishi Geoff
Thompson anazungumzia kitu kimoja kilichonigusa na kuamua kukileta kwako, huenda kwa namna moja au nyingine kikakugusa pia.
Kifupi anazungumzia nguvu ya malengo katika kufikia mafanikio.
Geoff ,
anazungumzia survey maarufu iliyofanyika
miaka mingi ya nyuma katika chuo kikuu cha Harvard, miongoni mwa vyuo bora
zaidi duniani. Survey ilihusu mambo
mbalimbali ambayo mwanafunzi alitakiwa kuyatolea maoni yake. Matokeo ya survey hiyo yalisababisha mshituko
mkubwa miongoni mwa wahadhiri wa Harvard hususani katika vipengere vifuatavyo;
- Una malengo?
- Una utaratibu wa kuandika malengo yako?
Karatasi
zilipokusanywa na majibu kupitiwa, wahadhiri walishangazwa. Wastani wa 15% ya
wanafunzi ndio waliojibu kuwa wana malengo yoyote, na kati kati yao pia ni wachache tu ndio waliojaribu
kuandika malengo yao.
Hii ina
maanisha kuwa zaidi ya asilimia 85 ya wanafunzi wote waliofanyiwa survey, walikuwa wanasoma bila malengo
yoyote. (Ikumbukwe kuwa Harvard hujivunia kudahili wanafunzi bora zaidi
nchini Marekani).
Pamoja na
kwamba survey hiyo iliwashangaza na
kuwakatisha tamaa wahadhiri wa Harvad, matokeo yalihifadhiwa.
Miaka mingi
baadaye, katika mkutano wa wafanyakazi wa chuo hicho, mhadhiri mmoja aliibua
wazo la kurudiwa kwa survey kama hiyo
ili kuona kama kuna tofauti ya wanafunzi waliokuwa wanadahiliwa muda huo na
kipindi cha nyuma.
Kabla
hawajakubaliana kuchukua survey
nyingine ulifanyika uamuzi wa kukusanya pesa kwa ajili ya kuwafuatilia
waliofanyiwa survey ya kwanza kama
kuna walichofanikisha maishani.
Wanafunzi
waliofanyiwa survey ya awali
walitafutwa. Wale walioandika malengo yao waliulizwa;
Umefanikisha malengo uliyojiwekea
kipindi ukiwa mwanafunzi?
Na wale
ambao hawakuandika malengo yao waliulizwa;
Maisha yako yanaendaje?
Cha
kushangaza, waligundua kuwa asilimia 95 ya wale ambao hawakuandika malengo yao
hawakufanikiwa chochote na hawakuwa wamefikia uhuru wa kifedha kama ilivyokuwa
inatarajiwa kwa mtu aliyehitimu chuo kikuu (hasa Harvard).
Asilimia 80
ya wale waliojiwekea malengo walikuwa wameyafanikisha na kwa wale wachache
ambao waliandika malengo yao walikuwa wamekwisha fanikiwa kufikia uhuru wa
kifedha.
Hapa
tunajifunza kuwa kujiwekea malengo ni utaratibu muri wa kufanikiwa maishani.
Watu wengi
tunapuuza kujiwekea malengo kwa kufikiri kuwa majina makubwa ya vyuo
tunavyosoma yatatufanya tufanikiwe. Pengine kwa kudhani kwa kuwa tunafaulu
mitihani yote tunayofanya, tutafanikiwa bila malengo kuwa na yoyote.
Au
tunafikiri kuwa tutafanikiwa kwa kuwa tunatoka katika koo na familia maarufu.
Kwa vyovyote
vile kujiwekea malengo ni muhimu kama unataka kufanikiwa.
Mtu asiye na
malengo ni sawa na meli au ndege inayoanza safari bila kujua inakoelekea.
Utawezaje kufika mahali ambapo hujui palipo? Huwezi kufika kama hujui
unakokwenda.
Unaweza ukaanzisha safari ndefu, ukavumilia
dhoruba kali kwa kuwa unafahamu unakokwenda, unapaona unakoelekea. Hata kama
mambo yatakuwa magumu vipi, utaangalia mbele na kusema, “ninaona mwnga mbele,
nimekaribia kufika.”
Hebu fikiria
unapigwa na dhoruba kali katika safari ambayo hujui unakoelekea, kishawishi cha haraka kitakuwa ni kurudi ulikotoka au kuelekea sehemu nyingine.
Bila malengo mbele
utaona giza na maluweluwe tu. Watu wengi tunakata tamaa na kushindwa kufikia
mafanikio kwa sababu hatuna malengo.
Unahitaji Malengo.
.jpg)
0 comments:
Chapisha Maoni